Video | Kufungiwa wimbo inauma, sikia tu kwa mwingine – Shaa mp4 | Free Download


Akiongea na Bongo5, Shaa ambaye video ya wimbo wake ‘Sugua Gaga’ ilifungiwa kuchezwa kwenye TV, amedai kuwa tena heri ifungiwe video tu, kuliko audio kama ilivyotokea kwa Chura ya Snura na Pale Kati ya Nay wa Mitego.
“Audio ndio kitu muhimu zaidi hapa Bongo, kila mtu ana redio, ni wachache sana wana muda wa kuangalia TV, ni wachache sana wanaweza kugharamia ving’amuzi,” anasema Shaa.
“Ni mara mia uwe na issue za video kuliko audio.”
Shaa anadai kufungiwa kwa kazi zao ni kitu kinachowagharimu sana.
“Hii ni kazi, hii ni biashara, ni sawa kwa mfano mimi nina perfume yangu hii hapa, nimewekeza hela halafu ikafungiwa, mtu hawezi kujua ni kitu gani, siwezi kuipost, siwezi kuitangaza, kwahiyo hiyo hela inakuwa imepotea.”
Shaa amedai kuwa alijihadhari tatizo kama hilo lisitokee tena kwenye kazi yake mpya aliochia sasa ‘Sawa’ na ndio maana aliirudisha video hiyo kwa Justin Campos ili ifanyiwa marekebisho.



Previous
Next Post »