Tambwe amesema tuzo ya mfungaji bora aliyopata itamuongezea ari ya kufanya vizuri kwenye ligi ya msimu ujao na kuinufaisha timu yake kufanya vizuri zaidi ya ilivyokuwa mwaka huu
Mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga, Amissi Tambwe amesema tuzo ya mfungaji bora aliyopata itamuongezea ari ya kufanya vizuri kwenye ligi ya msimu ujao na kuinufaisha timu yake kufanya vizuri zaidi ya ilivyokuwa mwaka huu.
Tambwe ameiambia Goal, siku zote anapokuwa uwanjani akili yake huwa inawaza kufunga na mafanikio hayo yanatokana na bidii zake anapokuwa mazoezini.
“Unajua Simba waliponiacha eti wakidai nimeshuka kiwango iliniuma sana lakini nawashukuru Yanga kwa kutambua uwezo wangu na nilipania kuwasaidia nashukuru nilimaliza nafasi ya pili msimu wangu wa kwanza nikiwa na Yanga lakini msimu uliofuata nilipambana na kufanikiwa kuwa mfungaji bora,”amesema Tambwe.
Mshambuliaji huyo amesema bado ataendelea kuichezea Yanga msimu ujao kwasababu ni timu ambayo imeonyesha kuhitaji mafanikio katika kufika mbali kwenye mashindano mbalimbali na yeye amejitoa kwa ajili ya kuipigania timu hiyo.
ConversionConversion EmoticonEmoticon