Ulaji wa matunda na mboga za majani unaweza kukusaidia kupata furaha, utafiti mmoja wa Australia umegundua. Watafiti hao wamegundua kuwa watu waliobadili mtindo wao wa ulaji, na kuanza kula matunda na mboga za majani kwa wingi katika mlo wao wa kila siku wamepatwa na ongezeko la kuwa na hisia za furaha na kuridhikaa kimaisha ikilinganishwa na namna ile ile ambayo mtu asiye na ajira anavyohisi mara apatapo ajira limeeleza jarida ‘la American Journal of Public Health.
Redzo Mujcic ambaye ni mtafiti mwenza wa afya na uchumi katika chuo kikuu cha Queensland nchini Australia amesema……..>>>”Ni wazi kuwa ulaji wa matunda na mboga za majani huongeza furaha yetu kwa kasi zaidi kuliko inavyoongezeka kutokana na afya ya muhusika’‘
Utafiti uliofanyika kabla ya huo ulionyesha kwamba kula mboga na matunda mengi kumesaidia mno kuimarisha sana afya ya miili ya watu, lakini faida kama hizo zinaanza kuonekana baada ya kipindi kirefu cha wakati, wamesema watafiti hao.
ConversionConversion EmoticonEmoticon