Shirikisho la Soka nchini Hispania, limetoa ratiba kamili ya mechi zitakazochezwa kwenye ligi kuu ya nchini humo msimu wa mwaka 2016/2017 zitakazoanza Agosti 21.

Mabingwa watetezi wa kombe hilo, Barcelona watapambana na Real Betis huku mabingwa wa kombe la Uefa, Real Madrid wakianza mechi yao ya kwanza na Real Sociedad.
Jumatatu ijayo timu ya Barcelona wataungana kwa pamoja kuanza mazoezi na baadaye wataenda nchini Uingereza kucheza baadhi ya mechi za kirafiki ikiwemo na timu za Celtic, Leicester City na kumalizia na timu ya Liverpool.
ConversionConversion EmoticonEmoticon