Simba imemleta nchini mshambuliaji Ndjack Anong Guy Serges raia wa Cameroon kutoka timu ya Panthere kwa ajili ya majaribio kabla ya kumsajili
Klabu ya Simba imemleta nchini mshambuliaji Ndjack Anong Guy Serges raia wa Cameroon kutoka timu ya Panthere kwa ajili ya majaribio kabla ya kumsajili.
Kocha Joseph Omog, ameiambia Goal, anahusika kwenye ujio wa mchezaji huyo kwasababu anamfahamu vizuri mchezaji huyo kutokana na uwezo aliokuwa nao wa kucheza nafasi ya ushambuliaji na winga.
“Nimchezaji mzuri namfahamu na mimi ndiyo nimehusika kumleta hapa kwa ajili ya majaribio kama ataonekana anafaa kuwa naye tutamsajili lakini nilipenda aanze na majaribio ili tujiridhishe uwezo wake,”amesema Omog.
Simba imeweka kambi mkoani Morogoro kujiandaa na msimu mpya na mbali na mshambuliaji huyo kuna wachezaji wengine wawili waliopo wanaofanya majaribio kwenye klabu hiyo iliyodhamiria kufanya vizuri msimu ujao.
ConversionConversion EmoticonEmoticon