Rais wa Sudan Kusini amtumia ujumbe wa shukrani Rais Magufuli




Ujumbe huo wa Rais Kiir umewasilishwa Tanzania na waziri wa biashara na viwanda wa nchi hiyo Stephen Dhieu Dau Ayik, kwa makamu wa rais Bi. Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Rais Magufuli jana ikulu jijini Dar es Salaam.
Waziri huyo amesema kwa sasa hali usalama inazidi kuimarika kufuatia kusitishwa kwa mapigano ya wanajeshi watiifu wa Salva Kiir na wanajeshi watiifu wa aliyekuwa Makamu wa rais Riek Machar.
Kwa niaba ya Rais Magufuli, Bi. Suluhu alisema, “Serikali ya Tanzania itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha amani inapatikana katika Taifa hilo changa barani Afrika ambayo itawezesha wananchi wa Taifa hilo changa barani Afrika ambayo itawezesha wananchi wa taifa hilo kufanya kazi kwa maendeleo kwa amani na utulivu.”
“kuna umuhimu wa kufanyika mazungumzo ya amani ya kutafuta suluhu ya mgogoro huo ili kukomesha vita ambavyo vimekuwa vikigharimu mali na maisha ya mamia ya watu wa Sudan Kusini,” aliongeza.
Makamu wa rais pia amezitaka pande zote mbili zinazopingana kuzingatia na kuheshimu mkataba wa amani waliosaini jijini Arusha mwaka 2015 uliolenga kusitisha vita vya wenyewe kwa wenyewe na kurejesha amani katika taifa hilo.
BY: EMMY MWAIPOPO

ConversionConversion EmoticonEmoticon

:)
:(
=(
^_^
:D
=D
=)D
|o|
@@,
;)
:-bd
:-d
:p
:ng