Magufuli azigeukia kampuni za simu


Moja ya habari iliyoripotiwa ni hii kutoka gazeti la Habari Leo yenye kichwa cha habari ‘Magufuli azigeukia kampuni za simu”
Gazeti la Habari Leo limeripoti kuwa Rais John Magufuli ameagiza kwa taasisi zinazosimamia fedha na kodi, kuhakikisha kuwa Serikali inakusanya kodi kwenye miamala ya fedha, inayofanya na taasisi hizo na kampuni za simu na za madini.

Aidha Gazeti hilo limeripoti kuwa Rais Magufuli ameagiza kuwa sh bilioni saba zilizolipwa na pensheni hewa, zirejeshwe mara moja huku akitoa  ufafanuzi wa hatua ya serikali ya kusitisha kwa muda ajira serikalini. Rais Magufuli aliyasema hayo Dar es salaam jana katika kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Previous
Next Post »