Kocha wa klabu ya Yanga Hans van der Pluijm amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuifundisha klabu hiyo Yanga.
Pluijm ambaye amekuwa na mafanikio makubwa na Yanga katika misimu yake miwili baada ya kuchukua ubingwa wa Tanzania Bara misimu yote hiyo.
Raia huyo wa Uholanzi, alichukuwa ubingwa wa Tanzania Bara msimu wa 2014-15 akiwa na mechi mbili mkononi, msimu wa 2015-16, akabeba akiwa na mechi tatu mkononi.
Msimu wa 2015-16 ameiwezesha Yanga kubeba ubingwa wa Kombe la Shirikisho Tanzania na kuiwezesha kufika hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho la Afrika.
ConversionConversion EmoticonEmoticon