Dr Dre akifungwa pingu na polisi nje ya nyumba yake


Rapper na producer mkongwe Dr. Dre wiki hii alikamatwa na polisi na kutiwa pingu nje ya nyumba yake huko Malibu baada ya kutokea kwa fujo na mtu asiyejulikana. Tukio hilo lilitokea barabarani.
Imebainika kuwa tukio hilo lilitokea nje ya nyumba yake na baadaye mtu mmoja aliripoti polisi kuwa Dr Dre alimtishia bunduki wakiwa barabarani. Dr Dre alikanusha, “Sikumtishia silaha, nilimuomba vizuri tu atoke mbele ya nyumba yangu sababu alizuia mahala napopitisha gari yangu.”
Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa mwendesha pikipiki huyo alimpigia Dr Dre kelele na baada ya polisi kufika mtu huyo alisema, “Here we go again, another black guy with a gun.”
Hadi polisi wanaondoka hakuna silaha yoyote iliyopatikana kwenye eneo hilo. Hata hiyo kesi hiyo ilikataliwa na mwanasheria wa Los Angeles.

ConversionConversion EmoticonEmoticon

:)
:(
=(
^_^
:D
=D
=)D
|o|
@@,
;)
:-bd
:-d
:p
:ng