Vanessa Mdee ni hot cake kwa sasa barani Afrika.
Wasanii kibao wanataka wamshirikishe, na wengine ni kutoka kwenye nchi ambazo ni ngumu kwa msanii wa Tanzania kuzipata. Moja ya nyimbo alizoshirikishwa ni ya msanii wa Ufaransa, Lylah na tayari video ya wimbo wao imeshafanyika.

Vanessa akiwa na msanii wa Ufaransa, Lylah
“Lylah ni msanii ambaye amekuwa akijaribu kuingia kwenye African market, anaimba Kifaransa na Kiingereza. So walifanya research they reached our team na nilivyokuwa Nigeria wakaja, wakapanga vitu vyote tukamalizia Nigeria,” Vee ameimbia Bongo5.
Pia Vee Money amedai ameshirikishwa na kundi kubwa la muziki la nchini Togo.
Anadai kuwa wimbo huo utampa nafasi ya kuimba muziki kwa Kifaransa, lugha ambayo anaijua vyema.
Anadai kuwa wimbo huo utampa nafasi ya kuimba muziki kwa Kifaransa, lugha ambayo anaijua vyema.
Hivi karibuni pia Vanessa aliingia studio kurekodi wimbo alioshirikishwa na msanii wa Malawi, Tay Grin.

Vanessa na Tay Grin
Bado ana collabo na Patoranking, Tekno na wasanii wengine wakubwa Afrika.
ConversionConversion EmoticonEmoticon