Desiigner ataja kiasi alichonunua beat ya ‘Panda’


Rapper wa Marekani Desiinger ambaye anafanya vizuri na single yake ya ‘Panda’, hivi karibuni alisema aliununua mdundo wa wimbo huo kwa kiasi cha dola $200 ambayo ni kama laki nne na nusu hivi za kibongo.
Desiinger anasema, “Nilikuwa gheto na washkaji zangu tukivuta bangi tu ndani ya nyumba huku tukicheza GTA [Grand Theft Auto] mara mshkaji wangu akapiga wimbo kutoka kwenye computer na kuniuliza kama naweza kuandika kitu kwenye mdundo huo nikamwambia naweza nikafanya hivyo, beat hiyo ilikuwa Youtube tu na baada ya siku mbili nikautoa wimbo huo.”
Previous
Next Post »