Hili ndiyo jibu la Pogba kwa timu zinazomnyatia


Mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa na klabu ya juventus, Paul Pogba ameziacha njia panda timu zinazomuania kwenye usajili unaoendelea barani Ulaya.

Pogba ambaye anawaniwa na klabu yake ya zamani ya Manchester United na Real Madridi huku thamani yake ya usajili ikionekana kuwa ni zaidi ya paundi milioni 100 ambayo itaweka rekodi ya usajili ya dunia.

Akihojiwa wakati wa utoaji tuzo za ESPY Awards, Pogba aliishika jezi ya Juventus ambayo ilikuwa mojawapo kati ya jezi tatu zilizowekwa mbele yake na akasema, “It’s my team, my family. It’s where I’m playing. When I wear this [shirt], I’m happy, I’m happy to play football. It’s something I’ve wanted to do since I was little. I’m happy here.”

Aidha mchezaji huyo alitania kwa kushika jezi ya United na kusema, “I don’t know them!” before adding: “It’s my first family.”

Alipoulizwa kuhusu timu ya Real Madrid, Pogba alijibu kwa kusema, “A great club.”

Pogba alimalizia kwa kusema kuwa kama akiambiwa achague ni klabu gani atachagua zote tatu ambazo ni Juventus, Madrid na Manchester United.
Previous
Next Post »