Zimetajwa sababu za noti ya shilingi mia tano kuchakaa mapema


Kumekuwa na malalamiko ya watu wengi kuwa noti ya shilingi mia tano haikai kwenye mzunguko muda mrefu hivyo huchakaa mapema, moja ya majibu yaliyotewa na benki kuu kupitia kwa afisa kurugenzi huduma za kibenki BoT, Patrick Fata ni kuwa noti hiyo ilitengenezwa ili ikae kwenye mzunguko kwa muda wa miezi saba na kingine ni kwa sababu inatumika sana………………
"noti ya mia tano inatumika kama chenji kwa hiyo inazunguka sana na kitu  kikitumika sana kina mwisho wake wa kuishi, kama noti ya shilingi mia tano tulitengeneza iishi miezi saba tu”
"tulitegemea iwe kwenye mzunguko miezi saba halafu irudi benki kuu, matokeo yake hairudi mpaka miaka minne au mitano kwa hiyo ule mzunguko unafanya ichakae haraka”
Previous
Next Post »