Shaa amedai kuwa ndoto yake ya kuwa na label yake mwenyewe imetimia mwaka huu.
Kwa sasa msanii huyo anafanya muziki chini ya label aliyoaianzisha, SK Musik. Kwa takriban miaka 10, Shaa alikuwa chini ya label ya MJ Records.
Anadai kuwa tofauti ya kuwa chini ya label ya mwingine na yake mwenyewe ni kwamba fedha inayopatikana inaenda moja kwa moja kwake kwa sasa ukilinganisha na mwanzo ambapo fedha kidogo aliyokuwa akipata ilikuwa ikikatwa na management.
“Finally sasa hivi nimepata recording label yangu mwenyewe inaitwa SK Musik, najisimamia mimi mwenyewe kwahiyo kipato asilimia kubwa kinarudi kwangu. MJ Records wanahusika sasa hivi hapa na pale, kunipa ushauri nini,” Shaa ameiambia Bongo5.
Shaa amedai kuwa kuanzia mwakani ataanza kusaini wasanii kwenye label yake ambao tayari ameshawapata. Amesema tofauti na label zingine ambazo zimekuwa zikiwaangalia wasanii wa Dar peke yake, SK Musik itawapa kipaumbele wasanii wa mikoani.
Amedai kuwa wasanii hao aliwapata wakati alipokuwa akizunguka mikoani kwenye media tour.
“Msanii wa kwanza nitakayeanza naye anatoka Tanga, msanii wa pili anatokea Dodoma, nimejaribu kidogo kuchukua watu wa mikoani.”
Wiki iliyopita Shaa aliachia wimbo wake wa kwanza chini ya SK Music, Sawa.
ConversionConversion EmoticonEmoticon