Imeripotiwa kuwa Manchester United ipo katika mchakato wa kutoa ofa rasmi kwa ajili ya kiungo wa Juventus Paul Pogba
Mustakabali wa Pogba umekuwa ukizungumziwa mno katika habari mbali mbali za uhamisho wa majira ya joto, United na Real Madrid zinaaminiwa kuwa klabu zinazitamani huduma ya Mfaransa huyo.
Sky Italia sasa kimeripoti kuwa United wanaandaa kitita cha paundi milioni 87 kama ofa kwa Juventus ili kuipata saini ya Pogba. Dau hilo litamfanya Pogba kuwa kiungo ghali zaidi katika historia ya soka.
Habari hizo zimeendelea kusema kuwa Pogba tayari ameshakubali vigezo na masharti kutua United na atakuwa akilipwa mshahara wa paundi milioni 10.92 kwa mwaka Old Trafford.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 alidumu miaka mitatu Manchester United kama mchezaji kati ya mwaka 2009 na 2012 kabla ya kuondoka kama mchezaji huru akiwa ameichezea timu ya wakubwa mechi saba tu.
Pogba atakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na Manchester United msimu huu baada ya Eric Bailly, Zlatan Ibrahimovic na Henrikh Mkhitaryan
ConversionConversion EmoticonEmoticon