Picha | Professor Jay achanganya Hip Hop na Kisingeli, amshirikisha Sholo Mwamba

Professor Jay
Professor akishuka uwanja wa fisi kwa ajili ya kuanza kushoot video hiyo
Msanii wa muziki wa Hip Hop na mbunge wa Mikumi, Professor Jay ameingia location wiki hii kushoot video ya wimbo wake mpya aliyomshirikisha msanii wa muziki wa kisingeli, ‘Sholo Mwamba’.

Rapper huyo ambaye anakuwa msanii wa kwanza wa Hip Hop kuchanganya ladha ya muziki wa Hip Hip na Kisingeli amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwa ajili ya ujio ya kazi hiyo.
Kupitia instagram, Professor Jay ameandika:
Kazi kazi video shooting. Kwa heshima kubwa sana tumeshoot video hii maeneo ya Manzese – Uwanja wa Fisi Tukiwapa tumaini jipya na nguvu wale wote waliokata tamaa na kuwaambia wakomae kwa kufanya kazi ipo siku mambo yatakuwa sawa. Kazi kazi . Professor Jay Featuring Sholo Mwamba.
Wimbo huo umeandaliwa na mtayarishaji Mesen Selekta na video imeongozwa na mtayarishaji wa video anayekuja kwa kasi, Travellah. Angalia picha za maandalizi ya video hiyo.
13709882_991767704275850_4749905384628379751_n
13709985_991768280942459_8028218776109747782_n

13718591_991767884275832_6013292265301977515_n

13729081_991768574275763_5339678413287727707_n

13729094_991768334275787_5504203818015636277_n

13754413_991768230942464_8863232886370455622_n

vv

vvd


13709882_991767704275850_4749905384628379751_n
Previous
Next Post »