Msanii wa muziki, Nedy Music, amesema haikuwa kazi rahisi kupata nafasi ya kusaini ndani ya label ya ‘PKP’ inayomilikiwa na mkali wa wimbo ‘Achia Body’, Ommy Dimpoz.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Usiende Mbili’, ameiambia Bongo5 kuwa alianza kumtafuta rais wa label hiyo ili afanye naye kolabo lakini akaambiwa aende akatafute management kwanza.
“Baada ya kufanya kazi zangu mbili binafsi, watu wangu wa karibu wakasema huwezi ukamtafuta msanii yeyote alafu ukamshirikisha kwenye wimbo wako mpya, nikasema huwezi kuandaa wimbo bila kujua ni nani utamshirikisha, kwa hiyo tukaangalia nani anaweza kufiti, tukachekecha tukaona bora tumuweke Ommy. Mimi nikaanza kumtafuta Ommy Dimpoz, nikaanza kumtafuta kwanza meneja wa Ommy, Mubenga, baada ya kuonana naye nikamweleza akasikiliza nyimbo zangu akasema tunaweza kufanya kolabo kwa sababu wimbo ulionisikilizisha ni mkali na nahisi pia Ommy atafanya vizuri, lakini baada ya kufanya hii kazi utaipeleka wapi na hauna management, kwa hiyo nikanibidi nirudi nyuma ili nikatafute management,” alisema Nedy
Aliongeza, “Lakini baada ya kukaa muda mrefu bila jibu ikanibidi nimweleze niliyopitia toka naanza muziki, nikamwambia kama kuna nafasi PKP ya kuwa msanii wenu naomba munisaini mimi nipo tayari, basi akaniambia nisubiri hawezi nijibu hapo hapo, siku hiyo nikapigiwa simu ili nikaonane nao na baada ya kukuta na Ommy Dimpoz nikaambiwa umefanikiwa kuwa msanii wa PKP, una vigezo vyote na kama kuna kitu hakiendi sawa tutakirekebisha,”
ConversionConversion EmoticonEmoticon