Bill Nas apanga kumtumia director wa nje kwenye video ya wimbo wake ujao


Msanii wa muziki wa Hip Hop Bongo, Bill Nass amefunguka kuwa atamtumia director wa nje kwenye video ya wimbo wake ujao.
Bill Nas ambaye kwa sasa video yake ya ‘Chafu Pozi’ inafanya vizuri kwenye TV na redio, ameiambia Bongo5 kuwa ataachia wimbo mpya mwezi Novemba na atamtumia director kutoka nje ya nchi kutengeneza video hiyo.
“Tumepanga kuachia wimbo mpya mwezi Novemba, kila mwaka ni ngoma mbili tu. Nahisi tunaweza tukaachia wimbo niliofanya mwenyewe bila kumshirikisha mtu,” alisema Bill Nas.
“Nahisi hii ngoma nyingine tutafanya na director mkubwa wa nje ili tuone tutasogea wapi na location itakuwa nje ya nchi pia,” aliongeza.
Previous
Next Post »