Yawezekana kabisa kuna matukio umeshawahi kuyasikia au hata kuyashuhuduia mwenyewe na yakakushangaza, basi hii pia liongezee kwenye hayo mengine, Hili ni tukio lililopata airtime kwenye Hekaheka ya Clouds fm leo July 14 2016.
Geah Habib katuletea hiI inayotokea Njombe Mbwa kuzaa Nguruwe.
Mbwa mmoja wa mkazi wa mtaa wa Kihesa maeneo ya Kilimani mjini Njombe amezaa mnyama aina ya Nguruwe, akielezea tukio hilo mke wake amesema kuwa waligundua kwamba mbwa huyo amezaa ngurume tangu juzi, baada ya mume na watoto wake kumjulisha hali hiyo na mara baada ya kushuhudia tukio hilo alitoa taarifa kwa uongozi wa mtaa huo pamoja na majirani huku akionesha kushtushwa na tukio hilo.
Daktari wa mifugo wa halmashauri ya mji wa Njombe, Anthony Mwangolombe mara baada ya kupata taarifa kuhusu suala hilo walifika eneo la tukio na amesema kuwa jambo hilo hajawahi kuliona likitokea kwa mbwa.
ConversionConversion EmoticonEmoticon