Alikiba na Barakah Da Prince wakutana na director Meji Alabi, video ya Nisamehe?


Alikiba na msanii mwenzake wa Rockstar4000, Barakah Da Prince wana kitu kizuri kinakuja kwaajili ya mashabiki wao.
ayari wimbo wa Barakah aliomshirikisha Kiba ‘Nisamehe’ ulishakamilika kitambo na huenda wawili hao wakawa wamekutana na muongozaji wa video wa Nigeria, Meji Alabi kwaajili ya kushoot video yake.
Alikiba ameshare video kwenye Instagram inayomuonesha akiwa kwenye gari na Barakah pamoja na muongozaji huyo. Kuna uwezakano mkubwa video hiyo ikafanyika nchini Afrika Kusini.
Meji ndiye aliyeongoza video za Alikiba, Chekecha Cheketua na Aje.
Barakah alitangazwa kuwa msanii mpya wa Rockstar4000 wiki kadhaa zilizopita na kuungana na Alikiba na Lady Jaydee kwenye label hiyo.
Previous
Next Post »