Young Dee akiri alikuwa akitumia madawa ya kulevya, aomba radhi na kuahidi maisha mapya



Rapper Young Dee hatimaye amethibitisha tetesi za miaka mingi kuhusu utumiaji wa madawa ya kulevya na kukiri kuwa ametumia kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu.
Akiongea na waandishi wa habari leo, Escape One jijini Dar es Salaam, rapper huyo amewaomba radhi watanzania kwa vitendo hivyo na kuahidi kubadilika.
Amedai kuwa ni marafiki ndio waliompoteza na kumuingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.
Amesema amepewa ushauri nasaha na wataalam na kwamba ameachana na matumizi hayo.
Pia rapper huyo amerejea rasmi kwenye uongozi wake wa zamani, Million Dollar Boyz, MDB alioachana nao mwaka jana.
13398965_259931741052515_1071474077_n
Young Dee na meneja wake Max Rioba
Kwa muda mrefu rapper huyo alikuwa akikanusha tetesi hizo.

ConversionConversion EmoticonEmoticon

:)
:(
=(
^_^
:D
=D
=)D
|o|
@@,
;)
:-bd
:-d
:p
:ng