Klabu ya Kagera Sugar ambayo makao makuu yake ni mkoa wa Kagera uwanja waKaitaba, usiku wa June 29 kumkia June 30 imetangaza kuwasajili nyota wapya watano kuelekea maandalizi yao ya kujenga kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi KuuTanzania bara.
Kagera Sugar kupitia account yao rasmi ya instagram wameandika ujumbe wa kuwakaribisha wachezaji watano, kwa maana ndio nyota wapya waliojiunga na kikosi hicho, nyota wapya waliotangazwa kusajiliwa ni Edward Christopher, Hassan Khateeb, David Burhan, Antony Matogolo na Themmy Felix Mnyama.

ConversionConversion EmoticonEmoticon