Samatta kaisaidia KRC Genk kutinga round ya pili ya Europa League


Mtanzania Mbwana Samatta bado anaendelea kufanya vizuri na kuzidi kuaminiwa na kocha wake Peter Maes ambaye kwa sasa amekuwa akimpa nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza na kucheza dakika zote 90, usiku wa July 21 2016 Mbwana Samatta aliichezeaKRC Genk mchezo wa pili wa Europa League dhidi ya Buducnost ya Montenegro.
Genk imecheza mchezo wake wa pili na kulazimishwa kucheza kwa dakika 120 na baadae mikwaju ya penati, dakika 120 zilimalizika kwa Buducnost kuongoza kwa goli 2-0, goli ambazo zilifungwa na Djalovic dakika ya 2 na Raickovic dakika ya 40 lakini mchezo uliamuliwa kwa mikwaju ya penati kutokana na KRC Genk kuibuka na ushindi kama huo katika mchezo wao wa kwanza.
Katika mikwaju ya penati Genk imefanikiwa kuibuka  na ushindi wa penati 4-2, penati za ushindi wa Genk zilipigwa na nahodha wao Thomas Buffel, HeynenMbwana Samattana Walsh, hivyo kwa matokeo hayo sasa Genk itacheza round ya pili ya Europa Leaguedhidi ya Cork City ya Jamhuri ya Ireland.
Previous
Next Post »