Maamuzi ya Chelsea kuhusu usajili wa kiungo N’Golo Kante


July 15 2016 miongoni mwa habari zilizobeba uzito katika headlines za usajili wa wachezaji katika kipindi hiki cha dirisha la usajili ni kuhusiana na kiungo wa kimataifa waUfaransa anayeichezea Leicester City ya England N’Golo Kante ambaye anahusishwa na kujiunga na Chelsea.
Taarifa kutoka Skysport na baadhi ya mitandao mikubwa ya soka duniani, imeripoti leo July 15 2016 Chelsea kukubaliana na Leicester City dau la usajili wa Kanteambalo linakadiriwa kufikia pound milioni 32, Kante mwanzoni kabla ya Euro 2016aliripotiwa kukataa ofa ya kujiunga na Chelsea ila sasa anaripotiwa kuwa weekend hii atafanya vipimo vya afya Chelsea.
Leicester-Training
Kante baada ya kufanya vipimo vya afya anaripotiwa kuwa atajiunga na Chelsea kwa mkataba wa miaka minne na baadae atasafiri hadi Austria walipoweka kambi Chelseakwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu England.
Previous
Next Post »